Je wewe ni mgonjwa lakini hauna stakabadhi na nyaraka rasmi za makao Ujerumani?
Tunatoa huduma za afya na matibabu bila malipo kwa watu wanaotafuta hifadhi nchini Ujerumani na wasiokuwa na haki ya makazi. Huduma zetu zinadumisha na kuzingatia usiri wa watu wote wanaotafuta ushauri na msaada kupitia shirika letu. Shirika letu ni huru na halina jukumu la kutoa habari zozote kuhusu wateja wake kwa mashirika mengine ya serikali na umma. Unaweza kuwasiliana na kupanga kukutana nasi kila Alhamisi, 16:00-17:30, Migrationszentrum Göttingen. Hatimayte, tutaweza kukuelekeza kwa (ma)daktari wa kuaminika.

Nambari ya simu: 0551/ 557 66 (masaa ya kazi)
Wakati wa dharuru: 0170 8457583

Migrationszentrum Göttingen
Weender Straße 42
37073 Göttingen